Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA: Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, ikiwemo ripoti zilizotangazwa kupitia mitandao ya ndani, imeelezwa kuwa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alijificha kwa muda wakati wa kile kinachoitwa “Operesheni Taco”.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Trump alidaiwa kujificha ndani ya gari maalum la kubebea vyakula na vinywaji (food and beverage wagon) akiwa ndani ya ndege ya Air Force One, kabla ya kuhamishwa kwa siri kwenda kwenye ndege ya kijeshi katika operesheni iliyofanyika kwa usiri mkubwa.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa uhamisho huo ulifanyika kwa haraka na kwa ulinzi mkali, huku hatua hiyo ikielezwa kuwa sehemu ya mpango wa kumhamisha bila kugunduliwa katika mazingira ya hatari ya kiusalama.
Maoni yako